Home Habari za michezo YANGA HAIBOI, HAIPOI, YATAMBULISHA BEKI MPYA KUTOKA ASEC MIMOSAS

YANGA HAIBOI, HAIPOI, YATAMBULISHA BEKI MPYA KUTOKA ASEC MIMOSAS

KLABU ya Yanga imemtambulisha beki wa kulia, Kouassi Attohoula Yao (26) kuwa mchezaji wake mpya wa tano kutoka ASEC Mimosas ya kwao, Ivory Coast.

Wachezaji wengine wapya wa kigeni Yanga ni winga Maxi Mpia Nzengeli kutoka Maniema ya kwao, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na beki wa kati Gift Freddy kutoka SC Villa ya kwao, Uganda.

Yanga pia imesajili wazawa wawili, beki wa kushoto Nickson Kibabage kutoka Singida Fountain Gate na kiungo JonΓ‘s Mkude kutoka kwa mahasimu, Simba SC.

SOMA NA HII  BRUNO GOMES NJIA NYEUPEEE KUTUA YANGA...KAZI ILIYOBAKI NI KWA NABI TU KUSEMA 'SU'...