KIPA wa Yanga Djigui Diarra ametakiwa kupunguza kujiamini zaidi awapo langoni jambo linaloweza kumtoa mchezoni na kujikuta akiisababishia timu yake matatizo.
Diarra kipa bora msimu uliopita alichangia kwa asilimia kubwa mafanikio ya Yanga akilitendea haki lango na kuwafanya wapinzani kutomchungulia mara kwa mara.
Akizungumza na Mwanaspoti kocha wa zamani wa makipa wa klabu hiyo Juma Pondamali alisema, Diarra ni kipa mzuri na anayajua majukumu yake tatizo lake kubwa ni hilo asipokifanyia kazi hatoamini kitakachomkuta.
“Unajua Diarra kujiamini kumezidi kipa anatakiwa kujiamini kiasi yeye kuchezea mpira vile siku akikutana na mchezaji mjanja ataharibu cv yake maana mashabiki wake hawatomuelewa na hapo imani kwake itatoweka kabisa aliangalie sana hilo,”
Alisema akijitahidi katika hilo anaweza kufanya makubwa kuliko aliyofanya msimu uliopita aliowazidi making bora akiwemo Aishi Manula wa Simba aliyeandamwa na majeraha kabla ya msimu kumalizika.
Pondamali alisema mbali uwezo wake wa kucheza kwa miguu anajua kupunguza goli na hiyi ni moja ya sifa iliyompa ubora.
“Mechi alizofungwa ni makosa madogomadogo sana , alikuwa anahokoa mipira mingi nje ya sita hilo jambo lilimbeba zaidi,” alisema Pondamali.
SOMA NA HII UONGOZI WA YANGA WAWAFARIJI WAATHIRIKA WA MAFURIKO HANANG......RAIS WA YANGA AFANYA HIVI