kipa wa simba
Habari za michezo

HUKO SIMBA MAMBO NI MOTO, KIPA MPYA HUYU HAPA KUTUA KABLA YA SIMBA DAY

Staff Desk August 3, 2023 2:11 pm

Klabu ya Simba imesema kuwa itamtangaza kipa mpya kabla ya kufikia siku ya Tamasha la Simba Day litakalofanyika Jumapili ijayo Agosti 6, 2023 katika Dimba la Mkapa.

Hayo yamesemwa na Meneja wa Habari na Mawasiliano Klabu ya Simba, Ahmed Ally ikiwa ni siku chache baada ya kuachana na aliyekuwa kipa wao, Jefferson Luis raia wa Brazil aliyedumu Simba kwa wiki moja tu tangu asajiliwe.

“Suala la golikipa tutatoa taarifa muda sio mrefu, kabla ya Tamasha la Simba Day kila kitu kitakuwa kimewekwa hadharani,” amesema Ahmed Ally.

Simba imeachana na golikipa Jefferson Luis aliyebainika kuwa na majeraha ambayo yatamuweka nje kwa muda mrefu.

Luis alisajiliwa hivi karibuni kama mbadala wa kipa namba moja wa Simba. Aishi Salum Manula ambaye yupo nje akijiuguza baada ya kufanyiwa upasuaji.

AHMED ALLY AFUNGUKA KUHUSU FUNGULIA MBWA YA YANGA, ALLY KIBA AHUSISHWA YANGA WAJA NA JIPYA KUHUSU MSIMU WA 2022/23 ISHU IKO HIVI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply