Habari za Simba SC
Habari za michezo

SIMBA WAPATA PENGO HILI KATIKA MCHEZO WA LEO

Staff Desk August 10, 2023 10:42 am

Kwenye mchezo wao wa kwanza wa Ngao ya Jamii leo Agosti 10, 2023, Simba SC watawakosa nyota wao wawili, Clatous Chama pampoja na Sadio Kanoute.

Akiuzungumzia maandalizi ya mchezo huo utakaopigwa kwenye dimba la Mkwakwani jijini Tanga, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ kocha wa Simba SC, amesema watawakosa nyota hao lakini anao nyota wengine watakaotimiza majukumu vizuri na kupata ushindi.

“Tumejiandaa kwa mchezo huu, tutawakosa nyota wawili lakini haliwezi kutufanya tushindwe kutimiza majukumu yetu ya kusaka pointi tatu,” alisema Robertinho.

Chama anaukosa mchezo huo baada ya kufungiwa mechi tatu na Bodi ya Ligi mwishoni mwa msimu uliopita huku Kanoute akipata kadi nyekundu katika mchezo wa Azam Sports Federation.

KAMA VIPI MJE NYIE, AZIZI KI, MZIZE WAFANYA BALAA YANGA IKIJIPIGIA TENA AZAM GAMONDI AFUNGUKA KILICHOOKOA JAHAZI DHIDI YA AZAM JANA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply