Habari za Simba
Habari za michezo

CHE MALONE AWA MWIBA KWA CHILUNDA NA PHIRI, ROBERTINHO AMPA NENO HILI

Staff Desk August 15, 2023 10:36 am

KAMA mashabiki wa Simba wakienda mazoezini wanaweza kutoa tuzo ya usajili bora kuwa beki kitasa Che Fondoh Malone, kwani jamaa kazi anaipiga sawasawa.

Unachokiona uwanjani basi hata washambuliaji wa Simba wanateseka sana mazoezini kila akimkaba mshambuliaji yoyote kocha wake Roberto Oliveira ‘Robertinho’anaibuka na maneno ‘excellent Che Malone’ yaani anamaanisha safi sana Che Malone.

Malone hapitiki hata mazoezini na hata washambuliaji wake wamekuwa wanapata shida kumpita kirahisi kutokana na utulivu wake.

Katika mazoezi ya juzi amekuwa mwiba akiwadhibiti washambuliaji kama Moses Phiri na Shabaan Chilunda kufika eneo la kipa wao.

Ubora huo wa mazoezini umemuweka katika daraja zuri la kuendelea kuaminika kwenye kikosi cha timu hiyo akiwa mtu muhimu kwenye safu ya ulinzi.

Robertinho akizungumzia beki huyo alisema ni beki anayejua sio tu kukaba Bali kuanzisha mashambulizi kuanzia nyuma.

“Che Malone ni beki mzuri sana nadhani kila mmoja anaona ubora wake, akili nyingi na nguvu kiasi unaona jinsi anavyojua kumsoma mshambuliaji anatulia lakini pia anaweza kuanzisha mashambulizi,” alisema Robertinho.

ROBERTINHO MTEGONI SIMBA….. ISHU IKO HIVI USAJILI WAGUSIWA BADO NI SIMBA, YANGA SASA NI KIGOMA UNAAMBIWA SIO POA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply