Yanga vs Aigles du Congo
Yanga SC

Yanga kuvaana na Aigles du Congo Wiki ya Mwananchi 2026: Kutambulishwa Mchezaji Mpya wa Mwisho!

Vardo August 7, 2026 10:45 am

Klabu ya Yanga SC imeweka wazi kuwa kilele cha Tamasha la Wiki ya Mwananchi kinachotarajiwa kufanyika Jumapili, Agosti 9, 2026, kitaambatana na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Aigles du Congo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Mchezo huo wa kukata na shoka utapigwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, ambapo Mabingwa hao wa Nchi watatumia fursa hiyo kuwatambulisha rasmi wachezaji wote wapya waliosajiliwa kwa ajili ya msimu wa 2026/27.

Mjarabu Mzuri wa Kujiandaa na Msimu Mpya

Akizungumzia maandalizi ya tamasha hilo, Msemaji wa Yanga, Ali Kamwe, ameeleza kuwa walipitia changamoto kubwa ya kupata mpinzani kutokana na klabu nyingi za kimataifa kuwa tayari zimeshapanga ratiba zao za kujiandaa na msimu mpya.

Licha ya ugumu huo, Kamwe amewahakikishia mashabiki kuwa Aigles du Congo itatoa kipimo stahiki na cha ushindani mkubwa kabla ya kuanza kwa ligi.

“Tumepata tabu kupata timu kwa sababu kila klabu imeshapanga ratiba zake, lakini tunawahakikishia Wana-Yanga tutapata mchezo mzuri na wa kiwango cha juu,” amesema Ali Kamwe.

Kutambulishwa kwa Mchezaji wa Mwisho wa Usajili

Mbali na burudani ya soka na shughuli mbalimbali za tamasha hilo, Kamwe amebainisha kuwa siku hiyo itakuwa na tukio jingine kubwa la kipekee: Yanga itamtambulisha rasmi mchezaji wake wa mwisho katika dirisha hili la usajili.

Tukio hilo litahitimisha rasmi shughuli za usajili za Yanga kwa msimu wa 2026/27, huku likiwawezesha Wananchi kushuhudia sura mpya zote zilizoongezwa kikosini ili kuimarisha timu hiyo.

Macho na masikio ya mashabiki wa soka nchini sasa yanaelekezwa Uwanja wa Uhuru siku ya Jumapili, kushuhudia kikosi hiki kipya kikianza rasmi safari yake ya kusaka mafanikio msimu huu.

Simba Yapeleka Ofa Wydad AC Kumsajili Selemani Mwalimu Jumla! Chama Atuma Ujumbe Mzito Simba SC: “Msimu Huu Ni wa Furaha Tu”