Habari za Simba SC
Habari za michezo

MABOSI SIMBA WAPEWA ZA USO….” HAWAJUI MPIRA….WANALETA SHIDA TU..”..

admin August 16, 2023 7:35 pm

Shabiki kindakindaki wa Klabu ya Simba, Yusuph Mwenda maarufu kama Mzee Mwenda anasema kuwa viongozi wengi wa timu hapa nchini hawaujui mpira, ambapo kawatolea mfano Viongozi wa klabu ya Simba SC.

Mwenda amesema hayo wakati akihojiwa na chombo kimoja cha habari kufuatia usajili wa kipa mpya wa Simba raia wa Morocco, Ayoub Lakred baada ya yule aliyesajiliwa awali, Jefferson Luis kurudi kwao kwa kukosa vigezo vya kucheza Ligi Kuu ya Tanzania.

“Kama hii juzi unamuacha Baleke nje, unamchezesha Bocco dakika 70 unaujua mpira? Kuna maelekezo huko nje ambayo yanatuharibia soka. Kocha anataka huyu mtu wangu acheze, hawa ndio wanatuharibia mpira, hawa ndio wanaovurunda, wawaachie wanaojua.

“Kocha ndiye alisema tukamletee wachezaji, wa nini sasa kama hawacheji? Viongozi wengi waliojichomeka kwenye uongozi wa soka kwenye hizi timu hawaujui mpira ni tofauti na wenzetu kule Ulaya. Mtu hajawahi kucheza mpira wala kuusoma lakini anapewa madaraka, anapokurupuka ndiyo inakwenda kuleta shida.

“Simba tulimsajili kipa wa daraja la nne, wakaja kusema heti ameumia, hakuna kitu kama hicho, ule ni ubabaishaji, mtu alikwenda tu hajui, sababu waliokabidhiwa lile rungu si wanamichezo. Walikwenda tu wakaburuta baadaye wakaigeuza stori,” amesema Mwenda.

Nini maoni yako?

KUELEKEA MECHI YAO YA CAF JUMAPILI HII…GAMONDI NA YANGA YAKE ‘WAMEZUKA’ NA HILI JIPYA… KUHUSU PHIRI KUKOSA  PENATI DHIDI YA YANGA …SIMBA WATOA TAMKO LAO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply