Home Habari za michezo SOKA LA GAMONDI LAWAIBUA MABOSI YANGA, ISHU IKO HIVI

SOKA LA GAMONDI LAWAIBUA MABOSI YANGA, ISHU IKO HIVI

Habari za Yanga leo

MABOSI wa Yanga wameumizwa na kitu kimoja tu juzi, kupoteza taji la Ngao ya Jamii ambalo walilishikilia kwa misimu miwili, lakini kuna kauli ya mamlaka wakaitoa juu ya kikosi chao.

Kauli hiyo ilitolewa na Makamu wa Rais wa timu hiyo, Arafat Haji akisema licha ya kupoteza taji hilo, lakini wako timamu wakiwa na matumaini na soka la kocha mpya, Miguel Gamondi.

Arafat alisema wameyapokea matokeo hayo kwa kuwa ndio sehemu ya ushindani, lakini uongozi wao uko pamoja na wachezaji na benchi la ufundi chini ya Gamondi kutokana na soka safi ambalo kikosi chao kinalicheza kwa sasa.

Kiongozi huyo aliongeza zaidi kuwa, wachezaji walikosa kuamua mchezo pekee ndani ya dakika 90 hasa mechi hiyo, ila wanafahamu kwamba wamewaachia maswali mazito wapinzani wao kwa timu yao jinsi ilivyocheza mechi mbili.

“Tumeumia kupoteza hii Ngao, lakini kiukweli tuna matumaini makubwa na timu yetu. Tungefungwa ndani ya dakika 90 tungesema kuna shida mahali, lakini sote tunafahamu penalti hazina mwenyewe,” alisema Arafat.

“Timu yetu imecheza mpira mkubwa. Tunajua (Simba) wanashangilia kuchukua Ngao, lakini kwenye mioyo yao wanajua ni namna gani waliteseka kwenye mchezo ule. Viongozi wao tulikuwa nao pale juu (jukwaani Uwanja wa Mkwakwani) tuliwaona.

“Tunajivunia sana wachezaji na makocha wetu. Tunafahamu walimu wamejua wapi kuna shida ili wakati mwingine tuimalize mechi mapema na jambo zuri hili limetokea mapema tutarudi na nguvu kubwa kwenye ligi.”

SOMA NA HII  KIUNGO YANGA ASAINI MIAKA MIWILI