Home Habari za michezo KISA KUVUNJIWA MKATABA…FIFA WAAMURU BANDA ALIPWE MAMILIONI…..

KISA KUVUNJIWA MKATABA…FIFA WAAMURU BANDA ALIPWE MAMILIONI…..

Habari za Michezo

BEKI wa Richardsbay FC au Natal Rich Boys, Mtanzania Abdi Banda ameshinda kesi aliyoifungua dhidi ya timu yake ya zamani Chippa United ambayo sasa inatakiwa kumlipa mamilioni ya pesa.

Kupitia kwa mwanasheria wake, Lyrique de Plessis raia wa England, Banda alifungua kesi FIFA kudai mkataba wake baada ya Chippa kuvunja mkataba wake kinyume na sheria.

Banda aliingia mgogoro na klabu hiyo baada ya kuitwa timu ya taifa, Taifa Stars Mei mwaka huu ambapo Chippa ilimtaka kupunguza mshahara wake kuanzia Juni Mosi jambo ambalo yeye alilikataa.

Akinukuliwa na gazeti la  Mwanaspoti kwa njia ya simu kutoka Afrika Kusini, Banda alisema kitendo cha kukataa kupunguza mshahara ni sababu ya waajiri wake kusitisha mkataba na kuamua kukimbilia FIFA.

“Mwanasheria wangu alifungua mashtaka Fifa na alihakikisha anapambana napata haki zangu baada ya kuona mkataba ulivunjwa kimakosa, tayari huku imetoka ikitaka Chippa inilipe stahiki zangu, nimefurahi sana kwa hilo,” alisema na kuongeza;

“Kilichofanywa na Chippa sikuwahi kukaa nao chini kukubaliana nao, ili mshara wangu upunguzwe zaidi ya wao kutuma barua iliyoelekezwa hivyo, hivyo halikuwa jambo jepesi kwangu, huenda linawapata na wachezaji wengine.”

Baada ya kushtaki na kabla ya kutoa hukumu hiyo, Fifa iliitaka Chippa iwasilishe barua ya utetezi wao kuhusu kesi hiyo Julai 18 huku hukumu yenyewe ilitarajiwa kutolewa rasmi Septemba 18, ila imewahi zaidi.

Pesa ambayo Banda anatakiwa alipwe kama fidia kutokana na kuvunjiwa mkataba huo bila makubaliano ni Randi 4.5 ambayo ni sawa na Sh600 milioni.

SOMA NA HII  TABIA ZA 'KIWAKI' ZAMPONZA MORRISON YANGA...NABI AMUONJESHA' JOTO YA JIWE'...