Home Habari za michezo JE’ KMC ATAENDELEA KUWA KIBONDE WA YANGA, KAMPENI INAANZA HIVI LEO LIGI...

JE’ KMC ATAENDELEA KUWA KIBONDE WA YANGA, KAMPENI INAANZA HIVI LEO LIGI KUU

Habari za Yanga

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara, Yanga leo inaanza kampeni ya kutetea taji hilo dhidi KMC.

Mchezo huo pekee wa ligi hiyo leo utafanyika uwanja wa Azam Complex, Chamazi Dar es Salaam.

Takwimu zinaonesha Yanga na KMC zimekutana mara kumi, mabingwa hao watetezi wakishinda mara saba, sare mara mbili na kupoteza mchezo mmoja.

Katika mchezo pekee wa Ligi Kuu uliopigwa Agosti 22, wenyeji Singida Fountain Gate imelazimishwa suluhu na Tanzania Prisons kwenye uwanja wa CCM Liti mjini Singida.

SOMA NA HII  RIVERS UNITED WAVAMIWA DAR...WAPULIZIWA SUMU...WAIBIWA MAMILIONI YA PESA