Home Habari za michezo ROBERTINHO ANACHOKIFANYA KWA MIQUISSONE NA CHAMA NI HATARI KWA WAPINZANI

ROBERTINHO ANACHOKIFANYA KWA MIQUISSONE NA CHAMA NI HATARI KWA WAPINZANI

KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Roberto Oliveira, ndani yake inasukwa pacha ya viungo wa kazi, Luis Miquissone na Clatous Chama kwa ajili ya mechi za kitaifa na kimataifa.

Kwenye mechi mbili za Ligi Kuu Bara msimu huu dhidi ya Mtibwa Sugar na Dodoma Jiji, tayari balaa la nyota hao limeanza kuonekana.

Katika mchezo dhidi ya Mtibwa uliochezwa Uwanja wa Manungu, Morogoro, Chama alianza kikosi cha kwanza, Luis alitokea benchi ambapo Chama alifunga bao dakika ya 80 kwa pasi ya Luis. Ubao ulisoma Mtibwa Sugar 2-4 Simba.

Dhidi ya Dodoma Jiji, Luis alitokea benchi kwa mara nyingine, akatengenezewa nafasi tatu na Chama, lakini zote alikwama kufunga mabao.

Miongoni mwa nafasi za dhahabu ambazo alitengenezewa Luis ilikuwa ni ile ya dakika ya 74. Licha ya kukwama kufunga timu ya Simba ilikomba pointi tatu kwa ushindi wa mabao 2-0.

SOMA NA HII  ORODHA YA WACHEZAJI 31 WA SIMBA WATAKAOCHEZA KIMATAIFA