Home news BAADA YA KUANZA KWA KASI YANGA…NKANE AKUTWA NA GONJWA LA AJABU..KUKAA NNJE...

BAADA YA KUANZA KWA KASI YANGA…NKANE AKUTWA NA GONJWA LA AJABU..KUKAA NNJE MPAKA….


KIUNGO Mshambuliaji waYanga, Denis Nkane atakuwa nje ya uwanja kwa mwezi mmoja kutokana na kusumbuliwa na Kinena.

Nkane alisajiliwa na Yanga kwenye dirisha dogo la usajili akitokea Biashara United, huku kwa sasa akiwa amecheza mechi mbili za michuano ya Mapinduzi.

Kiungo huyo aliumia kwenye mchezo wa hatua ya makundi dhidi ya KMKM kwenye Kombe la Mapinduzi.

Akizungumza na Gazeti la Championi , Daktari waYanga, Youssef Mohammed, alisema kuwa: “Kwa sasa kuna jumla ya wachezaji wanne ambao ni majeruhi kwenye kikosi.

“WapoYacouba Sogne, Kibwana Shomari,Abdallah Shaibu ‘Ninja’ ambao wanaenda Tunisia kwa ajili ya kupatiwa matibabu na Denis Nkane.

“Denis alipata majeraha kwenye mchezo wa mwisho wa makundi ambapo kwa sasa anasumbuliwa na Kinena, tatizo ambalo litamuweka nje kwa muda wa mwezi mmoja.”

SOMA NA HII  POINTI NNE ZA MBEYA ZAMPAGAWISHA MEXIME NA KAGERA SUGAR YAKE...MSIMAMO WAKE HUU HAPA...