Home Uncategorized BEKI WA YANGA MWAMNYETO AWAPOTEZA WOTE BONGO,ONYANGO,WADADA

BEKI WA YANGA MWAMNYETO AWAPOTEZA WOTE BONGO,ONYANGO,WADADA

 


BAKARI Mwamnyeto, nahodha msaidizi wa Yanga, ameweka rekodi ya dakika 810 ndani ya Ligi Kuu Bara kwa kuwapoteza mabeki wote ndani ya Bongo ambao aliingia nao kwenye fainali ya kusaka beki bora kwa msimu wa 2019/20 kwa kuruhusu mabao machache.

 

Mbali na safu yake ya ulinzi inayoundwa na pacha mwenzake Lamine Moro raia wa Ghana, Mwamnyeto pia ametumia dakika zote 90 ndani ya uwanja kwenye mechi zake nane ambazo alianza na kuwa ni chaguo la kwanza kwa makocha wote wawili.

 

Alianza kuwa chaguo la kwanza chini ya Zlatko Krmpotic ambapo alicheza mechi zote tano na chini ya Cedric Kaze ameanza mechi tatu na kumpoteza beki bora Nicolas Wadada wa Azam FC raia wa Ghana ambaye safu yake imeokota mabao manne na David Luhende wa Kagera Sugar safu yake imeokota jumla ya mabao 13.

 

Mbali na kuwapoteza nyota hao wawili ambao aliingia nao fainali, Mwamnyeto ambaye ni mchezaji wa zamani wa Coastal Union jina lake limo kwa wale wachezaji 27 wa timu ya Taifa ya Tanzania, ameipoteza na safu ya watani zao wa jadi Simba inayoongozwa na Joash Onyango ambao wameokota jumla ya mabao matano kwenye mechi 10.

 

Mpaka sasa timu zote zikiwa zimecheza jumla ya mechi 10, ni safu ya ulinzi ya Yanga imeruhusu mabao machache zaidi ambayo ni matatu huku safu ya ulinzi inayoongoza kwa kuokota mipira wavuni ni ile ya Mwadui FC inayoongozwa na Joram Mgeveke iliyookota mabao 20.

SOMA NA HII  ALLIANCE YAKWAMA KUFUTA UTEJA MBELE YA AZAM FC