Home Habari za michezo SIO SIMBA, SIO YANGA MAKOCHA HALI TETE NGAO YA JAMII

SIO SIMBA, SIO YANGA MAKOCHA HALI TETE NGAO YA JAMII

Yanga SC na Simba SC

WAKATI joto la fainali ya Ngao ya Jamii kati ya Yanga na Simba Agosti 13 likizidi kupanda, makocha wa timu hizo wametambiana kila moja timu yake kushinda mchezo huo wa watani wa jadi.

Wametoa tambo hizo jijini Tanga leo wakati wakizungumza na waandishi wa habari kuelekea kipute hicho kwenye uwanja wa Mkwakwani.

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema mchezo utakuwa mkubwa na mzuri kwa klabu yake hasa kwa mwanzo wa msimu na anajua umuhimu wa mchezo huo kwa kila timu.

“Ni Furaha kwangu kucheza mchezo huu mkubwa kesho, matarajio yetu ni kufanya vizuri na tumejiandaa bila presha yoyote kwasababu nimeshakutana na michezo ya aina hii mingi, tunaenda kupambana kwa ajili ya nembo ya Young Africans SC na Mashabiki wetu ambao wapo nasi kiła siku,” amesema Gamondi.

Naye Kocha Mkuu wa Simba Robertinho Oliveira amesema pamoja na ugumu wa mchezo huo klabu yake ipo tayari kushinda.

“Derby ni Derby na siku zote haitabiriki. Tunafahamu itakuwa mechi ngumu na tunaiheshimu Yanga lakini tupo tayari kuhakikisha tunashinda,” amesema Robertinho.

Kufika fainali Yanga imetoa Azam kwa mabao 2-0 wakati Simba imeondoa Singida Fountain Gate kwa mikwaju ya penalti 4-2.

SOMA NA HII  SIKU CHACHE BAADA YA KUONA MAZOEZI YA MBRAZILI...KAPOMBE AVUNJA UKIMYA SIMBA...