Home Habari za michezo STAA WA KIMATAFA AKOSHWA NA PIRA LA KIBU D….AFUNGUKA ANAVYOTESA MABEKI LIGI...

STAA WA KIMATAFA AKOSHWA NA PIRA LA KIBU D….AFUNGUKA ANAVYOTESA MABEKI LIGI KUU…

Habari za Simba SC

Ipo kauli moja inayosema ‘Muomba Mungu hachoki’ na ile inayosema mafanikio ya mtu yapo tu ila kuna siri kubwa mpaka mtu kufikia ndoto zako.

Kwa kila kijana hususan wachezaji wanakuwa na stori zenye kusisimua mpaka kufikia malengo yao.

Kiungo huyo wa zamani wa Azam FC ambaye msimu huu atakipiga Tala’ea El Gaish SC ya Misri kutoka Ghazl El Mahallah iliyoshuka daraja kutoka Ligi Kuu Misri ni Himid Mao.

Amefunguka mambo mengi ikiwa ni pamoja na maisha yake Misri akiweka wazi siku yake ya kwanza kuanza majukumu namna alivyochelewa mazoezini.

“Nilikutana na mazingira magumu miezi mitatu ya mwanzo hii ni kutokana na kuto kuzoea hali ya hewa na mazingira;

“Nakumbuka siku ya kwanza mazoezini nilichelewa kuamka kwasababu ya mazoea na nchi yangu ambapo tulikuwa tunafahamu muda wa kuamka. Nilichelewa dakika 15 zilinitoa mchezoni kwasababu sikujisikia vizuri kuanza na mguu mbaya,” anasema.

Himid anasema baada ya kuanza kuzoea alikuwa anaamka mapema na kufika kwa wakati mazoezini huku akithibitisha ukichelewa mazoezi unakatwa mshahara na hakuna masuala ya kuingia kambini kama Tanzania.

“Tukitoka mazoezini kila mtu anarudi kwake tunakutana siku moja kabla ya mechi ila kukiwa na mchezo nje ya uwanja wetu wa nyumbani ndio tunakutana siku mbili kabla ya mchezo kwaajili ya safari lakini tukitoka huko kila mmoja anarudi kwake,” anasema Himid ambaye pia anadai hata muda wa kukaa pamoja kuzungumza mambo nje ya soka ni lazima upangwe.

UKIONGEZEKA KILO UMEKWISHA

Soka la Tanzania linazidi kukua kadiri miaka inavyozidi kusonga ukitaka kuthibitisha hilo ni namna mastaa kutoka mataifa mbalimbali wanavyomiminika kuja kucheza lakini kuna vitu bado haviwabani kama anavyothibitisha Himid.

“Soka la kulipwa katika mataifa mengi yaliyoendelea lina vipengele vigumu mfano Misri nimecheza misimu sita sasa kuna vipengele vigumu sana tofauti na Tanzania;

“Kule mchezaji ukichelewa mazoezini, ukiongezeka kilo ukicheza michezo michache tofauti na makubaliano unakatwa mshahara, hayo ni makubaliano;

“Kitu kizuri ni kwamba kama umepewa mkataba na makubaliano ni kucheza basi una kila sababu ya kuhoji kwanini haupangwi wakati mkataba unakutaka ucheze hili ndio zuri kwa upande wetu nafikiri ndio maana hata mimi napata sana nafasi ya kucheza,” anasema kiungo huyo ambaye amekiri kuwa hajawahi kubaguliwa akiwa Misri.

KIBU NI MCHEZAJI WA KISASA

Kibu Denis ambaye anazungumzwa sana na mashabiki pale anapokosea tu, lakini akifanya vizuri hakuna anayemzungumzia lakini Himid Mao ameibuka na kumsifia mchezaji huyo.

“Kwasasa namkubali sana mshambuliaji wa Simba, Kibu ni mchezaji ambaye kila kocha anahitaji wachezaji aina kama yake hawezi kumuacha;

“Kibu ni aina ya washambuliaji ambao wanatumia nguvu na ni watata kwa mabeki ukikaa na mabeki ukawauliza hawawezi kuacha kumtaja kwasababu ana kasi na nguvu na mabeki hawapendi kukimbizwa sana,” anaongeza.

SOMA NA HII  BAADA YA KIMYA KIREFU....MWAKALEBELA AIBUKA NA JIPYA NDANI YA YANGA...ATAJA HUJUMA