Home Habari za michezo UONGOZI WA SIMBA WAKIANGUKIA KIKOSI CHA TIMU HIYO, KISA MATAJI YA MISIMU...

UONGOZI WA SIMBA WAKIANGUKIA KIKOSI CHA TIMU HIYO, KISA MATAJI YA MISIMU MIWILI…… WANENA MAZITO

Habari za Simba SC

Mabosi wa Simba wamekiangalia kikosi cha timu hiyo na kusema kikipata muunganiko na kurejesha soka lake, basi wapinzani watapata tabu sana kwani hawataacha kitu kutokana na malengo waliyojiwekea ya kurejesha kila taji walilopoteza misimu miwili iliyopita.

Simba ilipoteza mataji iliyokuwa ikishikilia misimu minne mfululizo ya Ligi Kuu Bara yaani Ngao ya Jamii na ASFC kwa watani wao, Yanga lakini wikiendi iliyopita ilirejesha Ngao kwa kuifunga Yanga katika fainali iliyopigwa Mkwakwani Tanga na hilo limewapa jeuri viongozi.

Mabosi hao kupitia Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ aliyekwenda Australia kushiriki kozi ya Diploma ya Uongozi, umesema kwa namna walivyojenga kikosi wanaona furaha inarejea upya Msimbazi.

Try Again alisema wana Simba wanatakiwa kujivunia uongozi makini unaowapa kile wanachokihitaji hivyo msimu huu wajiandae kupokea mataji waliyopoteza misimu miwili iliyopita na wameanza na Ngao wakati timu haijapata muunganiko mzuri uwanjani.

“Mipango yetu ni mingi sana. Tunaifanyia kazi kama unavyoona tumeanza na lengo kubwa ni kuhakiki tunairejesha heshima yetu ambayo tumeipoteza miaka miwili nyuma,” alisema Try Again na kusisitiza kuwa furaha ya wana Msimbazi inatokea kwa uongozi kufanya kinachohitajika kuanzia benchi bora la ufundi hadi wachezaji watakaowafikisha katika malengo yao.

“Ndio maana tumesajili watu kwelikweli, wenye uwezo mkubwa ambao tunaamini kwa uwezo wa Mungu mambo yataenda kama tulivyopanga na wana Simba watafurahia,” alisema Try Again aliyefafanua yupo Australia kwa kozi ya wiki mbili iliyoanza Agosti 8-22 na anaamini ataiva katika masuala ya uongozi hasa wa klabu.

“Huku nimekutana na watu mbalimbali ambao ni viongozi wenzangu, lakini kizuri zaidi nimeongea mengi na Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa), Gianni Infantino anayeifahamu Simba kutokana na ushiriki wake mzuri katika michuano ya kimataifa.”

Alisema, mbali na Infantino pia amebadilishana mawazo na mkurugenzi wa Mendeleo ya Soka wa Fifa, Ornella Bella kujadili kuhusu African League itakayofunguliwaTanzania ambayo Infantino atahudhuria. Alisema anaamini kozi hiyo itamfunua namna ya kuratibu mashindano makubwa na uongozi.

SOMA NA HII  BADI YA KARIAKOO YAZUA MASWALI MAKOCHA WAWEKEANA BIFU