Home Habari za michezo YANGA YA MSIMU HUU NI HATARI CHEKI ILICHOFANYA KWENYE MECHI ZA KUJIPIMA...

YANGA YA MSIMU HUU NI HATARI CHEKI ILICHOFANYA KWENYE MECHI ZA KUJIPIMA LEO

Habari za Yanga

Yanga imeendelea na maandalizi yake kuelekea msimu ujao ambapo leo itakuwa na mechi mbili za kirafiki za kujipima nguvu.

Asubuhi ya leo Yanga imecheza na timu ya Friends Rangers ya jijini Dar es Salaam na mabingwa hao wa Ligi Kuu msimu uliopita wakishinda kwa mabao 6-1.

Mabao ya Yanga yamefungwa na washambuliaji Crispin Ngushi aliyefunga mara mbili, Clement Mzize na Hafiz Konkoni, Pacome Zouzoua na Stephanie Aziz KI.

Konkoni huo ni mchezo wake wa kwanza wa kirafiki tangu asajiliwe na Yanga wiki iliyopita akianza vyema kwa kufunga bao hilo.

Leo tena jioni Yanga itacheza mchezo mwingine wa pili wa kirafiki watakapokutana na JKU ya Zanzibar.

Kabla ya mechi hiyo ya JKU Yanga imeshacheza mechi nne za kirafiki wakishinda zote ambapo mchezo wa kwanza ulikuwa dhidi ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini (1-0), Magereza Dar (10-0), Friends (6-1) na kufanya timu hiyo kufunga jumla ya mabao 17 huku wao wakiruhusu bao 1.

Yanga imeweka Kambi yake ya maandalizi kambini kwao AVIC TOWN Kigamboni huu ukiwa msimu wa pili sasa wakijiandaa eneo hilo hilo.

SOMA NA HII  PHIRI AJIKUTA NJE YA LIST.... ISHU NZIMA IKO HIVI