Home Habari za michezo GAMONDI AFUNGA PRE-SEASON YANGA KIBABE….. JUMATATU TANGA HAPAKALIKI

GAMONDI AFUNGA PRE-SEASON YANGA KIBABE….. JUMATATU TANGA HAPAKALIKI

Habari za Yanga SC

Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuhitimisha ratiba yake ya pre-season mwishoni wiki kabla kuelekea mkoani Tanga kwa ajili ya mchezo wa nusu fainali Ngao ya Jamii dhidi ya Azam Fc.

Mchezo huo utapigwa Jumatano, Agosti 9, katika uwanja wa Mkwakwani.

Yanga inatarajiwa kuhitimisha pre-season kwa mchezo mmoja wa kirafiki ambao utapigwa Avic Town.

Awali mabingwa hao wa Tanzania Bara walikuwa na ratiba ya kucheza mechi moja ya kirafiki uwanja wa Azam Complex, hata hivyo mpango huo hautakuwepo baada ya mapendekezo ya Kocha Miguel Gamondi.

Gamondi hayuko tayari vijana wake wacheze mechi ikarushwa mbashara kabla ya Ngao ya Jamii kwani kufanya hivyo ni kuwaonyesha wapinzani wake silaha

Gamondi anataka kuwasurprise wapinzani wake kwa kuwashushia kikosi na mbinu ambazo hawakuzifahamu kabla.

Hata Azam Fc ambao wana ratiba ya kuchuana na Bandari Fc Jumamosi katika uwanja wa Azam Complex, awali mchezo huo ulitangazwa kuwa ungeonyeshwa mbashara na Azam TV, lakini kulingana na taarifa iliyotolewa na Azam Fc, hautaonyeshwa na pia mashabiki hawataruhusiwa.

Kwa mujibu wa ofisa habari wa Yanga, Ally Kamwe Yanga wanatarajiwa kuelekea jijini Tanga siku ya Jumatatu ijayo, Agosti 7, 2023 tayari kuwakabili Azam Fc siku ya Jumatano.

SOMA NA HII  RATIBA YA KUAGA MWILI WA HANSPOPE