Tetesi za Usajili Simba
Habari za michezo

ROBERTINHO ATAMBA KUIKALISHA AL AHLY, AWEKA MTEGO HUU KWA MKAPA

Staff Desk September 5, 2023 11:53 am

KOCHA Mkuu wa Simba, Mbrazili, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amesema hana hofu ya kukutana na Al Ahly ya Misri, kwani anazijua mbinu zote wanazotumia.

Timu hizo zinatarajiwa kukutana katika mchezo wa kwanza wa CAF African Football League unaotarajiwa kucheza Oktoba 20, mwaka huu.

Mchezo huo wa robo fainali ya kwanza unatarajiwa kupigwa Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam kabla ya kwenda kurudiana Misri.

Akizungumza na Spoti Xtra, Robertino alisema kuwa mara baada ya droo ya michuano hiyo kuchezeshwa na wao kukutana na Al Ahly, haraka alianza kuwafuatilia kwa karibu wapinzani wao hao.

Robertino alisema amewafuatilia kwa kupitia video za michezo ambayo wameicheza msimu huu kwa lengo la kuwafahamu wachezaji hatari, hivyo tayari amewafahamu.

“Wapinzani wetu Al Ahly wana wachezaji wengine wazuri na hatari wa kuchungwa, lakini hiyo hainifanyi niwaogope, kwani na sisi tuna wachezaji wakubwa na hatari,” alisema Robertinho.

MAXI APIGWA STOP YANGA….. MAYELE AMPA NENO……. ROBERTINHO AIPA KIBURI SIMBA SC BEKI HUYU WA SIMBA ATIMKIA UARABUNI, ISHU IKO HIVI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply