Home Habari za michezo YANGA -TUNATAKA CHANGAMOTO YEYOTE….. ANAETUWEZA AJE…

YANGA -TUNATAKA CHANGAMOTO YEYOTE….. ANAETUWEZA AJE…

ALI KAMWE LOLOTE LITAFANYIKA MWARABU AFE...TUNGULI RUKSA...DUA RUKSA

Klabu ya Yanga imesema kuwa wakati huu ambapo ligi imesimama wanataraji kucheza mchezo wa kirafiki siku ya Jumapili lakini jina la timu bado halijawekwa hadharani.

Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe amesema pia wanatoa nafasi kwa timu yoyote ambaoyo wanajiona kuwa wana uwezo wa kushindana na Yanga basi wacheze mahala popote pale.

Akizungumza Ally Kamwe amesema;

“Tunatarajia kuwa na mchezo wa kirafiki siku ya jumapili. Tutatangaza tunacheza na timu gani. Hata hivyo tunatoa fursa kwa timu yoyote inaweza kuomba mchezo wa kirafiki na sisi tutacheza popote pale”

SOMA NA HII  BENCHIKHA AFUNGUKA WALIKIPATA BAADA YA KIPIGO KUTOKA KWA WYDAD