Home Habari za michezo KUELEKEA MICHUANO MIPYA YA CAF….MABOSI SIMBA ‘WAMWACHIA MSALA’ MBRAZILI…

KUELEKEA MICHUANO MIPYA YA CAF….MABOSI SIMBA ‘WAMWACHIA MSALA’ MBRAZILI…

Tetesi za Usajili Simba

UONGOZI wa Simba, umesema kulingana na usajili mkubwa waliofanya hawaoni sababu ya kutofanya vizuri katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika chini ya kocha wao, Mbrazil, Robert Oliveira ‘Robertinho’.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Simba, Salim Abdallah ‘Try Gain’ baada ya kujuwa wapinzani wao wa hatua ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Power Dynamo ya Zambia pamoja na Al Ahly katika michuano ya Afrika Supa Ligi.

‘Try Again’ alisema dhamilia yao ni kushinda mataji ya ndani na kufika hatua nusu faianlia ya Afrika pamoja na kushindana katika michuano mikubwa ya AFL.

Alisema benchi la ufundi linaloongozwa na kocha Robert Oliveira ‘Robertinho’, anafanya kazi yake kwa umakini baada ya kumpatia kila kitu ikiwemo usajili wa wachezaji wenye uwezo na uzoefu mkubwa wa michuano ya Afrika.

“Tumefanya usajili mkubwa sana kupitia dirisha kubwa la usajili mwaka huu na ukweli ni kuwa miongoni mwa sababu kubwa ni ushiriki wetu wa mashundano mbalimbali ikiwemo ya AFL, tumejipanga kushindana katika michuano yote mikubwa kufikia malengo yetu,” alisema Try Again.

Aliongeza kuwa wanaozoefu mkubwa wa mashindano ya kimataifa, tunaenda kucheza na Power Dynamos kusaka ushindi kwa mechi zote mbili na kutinga hatua ya makundi na michezo hiyo kuwa sehemu ya maandalizi dhidi ya Al Ahly.

“Wanatambua ugumu wa michuano iliyopo mbele yao na anaimani Robertinho anaendelea na maandalizi kufikia malengo yetu, kushinda kila mechi iliyopo mbele yetu, hatutaki kwenda kushiriki tunataka kuwa miongoni mwa timu zinazokwenda kushindana na klabu kubwa ikiwemo Al Ahly na zitakazokuwa mbele yetu,” alisema Mwenyekiti huyo.

Alisema wanaimani kubwa na benchi la ufundi na wachezaji kufanikisha malengo yao kwa sababu, wameanza vizuri msimu huu kutwaa taji la Ngao ya Jamii kwa kumfunga Yanga.

“Huu ni mwanzo mzuri kwetu, ukiangalia tulianza na taji la Ngao ya Jamii, tumecheza vizuri mechi mbili za ligi kwa kushinda, sasa nguvu zetu tunaendelea nazo kwenye ligi ya Mabingwa Afrika na AFL,” alisema Try Again.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATANO