Habari za Simba
Habari za michezo

KIEMBA:- “SIMBA WAMECHEZA MECHI NYEPESI SANA…”,HUWEZI KUMFUNGA AL AHLY KIRAHISI HIVYO…

admin September 7, 2023 7:50 pm

Mchambuzi wa soka nchini Amri Kiemba amesema mechi mbili za kirafiki alizocheza Simba SC ni nyepesi kulinganisha na mashindano yaliyopo mbele yao.

Mchambuzi huyo ameenda mbele zaidi kwa kusema kuwa, licha ya kuwa ni nyepesi lakini ina maana kwa mwalimu Roberto Oliviera ‘Robertinho’.

“Ni mechi nyepesi kulinganisha na michuano ambayo wanacheza lakini kiualimu inasaidia kutengeneza kile ambacho unataka kutokana na ushindani mdogo ina maana kama washambuliaji wako wamepoteza uwezo wa kufunga wanaweza kufunga na kuanza kugain kujiamini.

“Inawezekana mwalimu ana wazo lakini wachezaji hawamini katika ilo wazo lakini kama mnacheza na timu za kati inafanya wachezaji wazoee hizo mbinu, kama mnacheza mechi ngumu na mnafungwa inaleta ugumu kwa wachezaji kuamini hizo mbinu na kufanya mpango kufeli,” alisema Kiemba.

Simba wamecheza dhidi ya Cosmopolitan FC na kushinda 5- 1 lakini awali pia walicheza na Kipanga FC wakashinda 3-0.

ACHANA NA KUPEWA FREE BET MPAKA 200…PIRATES LEGACY INAKUPA USHINDI MARA 120 YA DAU LAKO… “KIBURI NA JEURI VIMEMFIKISHA NAVATUS ULAYA….WACHEZAJI WA KIBONGO WAVIVU…”

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply