Habari za Yanga
Habari za michezo

BALAA LA MAXI NZENGELI JANGWANI ‘LAMRUDISHA’ MAYELE YANGA….ATAJA HOFU YAKE…

admin September 7, 2023 9:49 am

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Yanga, Fiston Mayele, amesema kwa namna anavyomfahamu Maxi Nzengeli, anaamini nyota huyo ataisaidia sana timu hiyo kwa kubeba ubingwa msimu huu.

Mayela ambaye aliitumikia Yanga kwa misimu miwili, ameondoka kikosi hapo hivi karibuni na kutua Pyramids ya Misri, huku Nzengeli akiwa ni usajili mpya ndani ya Yanga. Nyota hao wote ni raia wa DR Congo.

Mayele aliweka wazi kuwa, anamfahamu vizuri Maxi, hivyo hana hofu na msaada wake ndani ya Yanga, anaamini kama ataendelea kupewa nafasi basi ataibeba zaidi timu hiyo.

“Maxi ni kati ya wachezaji wenye uwezo mzuri sana wa kufunga, hivyo sina shaka na alichoanza kukionesha, kikubwa anahitaji nafasi tu ya kucheza zaidi ya hapo,” alisema.

Maxi msimu huu katika michuano yote ambayo Yanga imecheza, tayari amefunga mabao manne, mawili Ligi ya Mabingwa Afrika na mengine Ligi Kuu Bara.

UWEZO WA KRAMO WAMUIBUA KIGOGO WA SIMBA….AFUNGUKA A-Z YANAYOENDELEA… MCHAMBUZI:- TUSIJIDANGANYE…TAIFA STARS NI WAKAIDA MNOO MBELE YA ALGERIA….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply