Home Habari za michezo KARIA:- YANGA WATASHIRIKI AFRICAN FOOTBALL LEAGUE MWAKANI…

KARIA:- YANGA WATASHIRIKI AFRICAN FOOTBALL LEAGUE MWAKANI…

Habari za Yanga SC

Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Wallace Karia amesema mwakani 2024 kupitia mashindano ya African Football League (Super League) Yanga itakuwa moja wapo ya timu zitakazoshiriki kwani wanategemea kuwa na timu 24.

“Kwa mwaka huu tuna timu nane lakini makubaliano ni timu 24, ukanda wa CECAFA na COSAFA tunatakiwa kutoa timu nane mwakani hata Yanga itakuwepo,”

Karia pia amewapongeza maofisa habari wa timu zinazoshiriki michuano ya CAF ngazi ya klabu Ally Kamwe (Yanga), Ahmed Ally (Simba) na Hussein Massanza (Singida Fountain Gate) kwa kuungana kwa pamoja katika kufanya hamasa kuelekea katika michezo yao.

Aidha amezitaka klabu hizo kwenda kuwakilisha nchi vyema kwani katika mashindano ya kimataifa nchi ndio inashiriki.

“Naamini timu zetu zitafanikiwa kuingia makundi katika mashindano ya kimataifa na hayo ndio malengo yetu, Timu zinapocheza mashindano ya kimataifa tunaenda kama Tanzania tukirudi kwenye ligi yetu kila mtu apambane”

MASTAA WANNE EL MERRIKH MIKONONI MWA GAMONDI.

YANGA ni wajanja sana baada ya kufanikiwa kuwanasa mastaa wanane hatari wa Al Merrikh ya Sudan baada ya Kocha wa timu hiyo, Miguel Angel Gamondi ya kuwafuatilia nyota hao walikuwa katika timu ya Taifa ya Sudan.

Kikosi cha Sudan kilichocheza na DR Congo na kufungwa mabao 2-0, kilikuwa na wachezaji wanane wa Al Merrikh katika mchezo wa kufuzu fainali za kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2023, zitakazofanyika Ivory Coast.

Mastaa hao wa Al Merrikh waliocheza Mohamed Mustafa, Ramadan Agab, b Bakhit Khamis na beki wa kati Mohamed Karshoum aliyecheza sambamba na beki wa Al Hilal, Mohamed Ahmed.

Wengine ni Ahmed Mahmoud na Mohamed Shambaly ambaye alitokea benchi na kati ya mastaa hao walioanza kikosi cha kwanza cha Al Merrikh ni kipa Mustapha, Agab, Kashroum na Shambaly ambao wana uhakika wa kuivaa Yanga Jumamosi hii, katika mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Afrika jijini Kigali.

Taarifa , kutoka ndani ya kambi ya Yanga kuwa Kocha wa Yanga, Miguel Angel Gamond aliufatilia mechi hiyo ya taifa ya Sudan na DR Congo kwa ajili ya kuwaangalia nyota wa Al Merrikh.

“Wikiendi iliyopita ( Septemba 9, mwaka huu), Kocha Gamond aliifatilia mechi kazi kubwa aliwaangalia nyota wa Al Merrikh waliocheza, amegundua kitu na kuwaeleza wachezaji wake jinsi gani ya kucheza katika mchezo huo hasa kwa ubora wa mchezaji mmoja mmoja wa wapinzani wetu,” alisema chanzo hicho.
Kocha Gamond alisema maandalizi yamefanyika vizuri kitu muhimu kwao kwanza ni kujiandaa vizuri kwa ajili ya kukabiliana na wapinzani wao hao kwa kupata matokeo mazuri ugenini.

Alisema Al Merrikh ni timu kubwa na imekuwa na wachezaji wazuri ambao wataingia kwa tahadhari kubwa kwenye mchezo huo ili kufikia malengo yao ya kupata ushindi ugenini kabla ya kurudiana nyumbani.

“Tunazo taarifa za Al Merrikh, baadhi ya mastaa wao wapo kwenye timu ya taifa ya Sudan, tunafahamu hata zile mechi walizocheza Kigali baadhi ya nyota wao hawapo, tutaendelea kufuatilia taarifa zao muhimu,” alisema Kocha huyo.

Aliongeza kuwa baadhi ya taarifa za wachezaji walizipata wameanza kuzifanyia kazi ikiwemo ubora wa mchezaji mmoja mmoja kuhakikisha wanakuwa makini katika mechi yao ya Jumamosi.

Kikosi cha Yanga kimesafiri jana mchana kuelekea nchini Rwanda na tayari kwa mchezo huo utakaopigwa katika Dimba la Pele, uliopo, Kigali, Nchini humo

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI ZA KUFUZU ‘AFCON 2023’...TAIFA STARS HAWATAKI MZAHA AISEE...WAAMUA KUTUMIA MBINU ZA SIMBA....