Home Habari za michezo MAFURIKO YA RWANDA YANGA WAFANYA HAYA

MAFURIKO YA RWANDA YANGA WAFANYA HAYA

Habari za Yanga

Rais wa Yanga SC, Hersi Said @caamil_88 na baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya timu hiyo wametoa msaada kwa waathirika wa mafuriko Magharibi mwa nchini Rwanda.

Viongozi wa @yangasc wametoa msaada huo wakiwa pamoja na viongozi wa timu ya APR FC ya Rwanda.

Hersi amesema Yanga SC inatambua uwepo wa mashabiki na wapenzi wa mpira wa Tanzania nchini Rwanda, lakini pia wamewaalika APR FC kama wenyeji wao kwa sababu ya heshima wanayoinesha kwa Yanga SC.

Yanga SC wamekuwa na utamaduni wa kutoa misaada katika sehemu mbalimbali wanayokwenda kwa ajili ya mechi zao.

Kikosi cha Yanga SC kipo hapa Rwanda kwa ajili ya mchezo wao wa kutafuta nafasi ya kuingia hatua ya Makundi ya Kombe la Klabu Bingwa Afrika na kesho watacheza dhidi ya Al Merrikh ya Sudan.

SOMA NA HII  TAIFA STARS, YANGA KUWANIA TUZO ZA CAF MSIMU HUU.....SIMBA 'WABANIWA'....