Home Habari za michezo GAMONDI AJA NA MSIMAMO HUU KWENYE SHEREHE ZA YANGA

GAMONDI AJA NA MSIMAMO HUU KWENYE SHEREHE ZA YANGA

Habari za Yanga SC

Kocha Mkuu wa Young Africans, Miguel Gamondi amesema pamoja na ushindi walioupata juzi dhidi ya Al Merreikh ya Sudan lakiní bado wana kazi ya kufanya ili kujihakikishia kutinga hatua ya makundi ya michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ikiwa ugenini nchini Rwanda juzi Jumamosi (Septemba 16) Young Africans ilibuka na ushindi wa mabao 2-0, matokeo ambayo yamewafanya kutanguliza mguu mmoja katika hatua inayo fuata ambayo ndiyo lengo kuu la timu hiyo kwenye michuano hiyo.

Kocha huyo kutoka nchini Argentia alisema haikuwa rahisi kupata ushindi huo kwani wenyeji wao Al Merreikh ni timu yenye uzoefu mkubwa katika michuano hiyo hivyo bado wanayo kazi ya kufanya kwenye mechi ya marudiano.

“Sioni sababu ya kuendelea kusherekea ushindi wakati bado tuna dakika 90 nyingine, nimewaambia wachezaji wangu waache kufikiria matokeo hayo na akili zao wazielekeze kwenye mchezo wa marudiano sababu AI Merreikh ni timu nzuri na watakuja na mbinu mpya ili kupindua matokeo,” alisema Gamondi.

Kocha huyo alisema ushindi wao wa juzi Jumamosi (Septemba 16) dhidi ya miamba hiyo ya Sudan ulitokana na kukitumia kipindi cha kwanza kuwasoma vizuri wapinzani wao ambao katika mchezo huo walicheza zaidi kwa kujilinda na kutumia mashambulizi ya kustukiza.

Alisema kwa kiasi fulani iliwasumbua kwa sababu licha ya kumiliki mpira na kutengeneza nafasi nyingi za mabao lakini iliwapa tabu washambuliaji wake kwakua wapinzani wao walijazana kwenye mdomo wa lango lao.

Kwa upande wake, Kocha Mkuu wa Al Merreikh, Osama Nabieh, alikiri timu yake kuzidiwa kimbinu na wapinzani wao Young Africans lakini akasema bado wanayo nafasi ya kucheza hatua ya makundi kwa kupindua matokeo kwenye mchezo wa marudiano utakaochezwa Septemba 30, katika Uwanja wa Azam Conplex, Dar es salaam.

SOMA NA HII  BODI YA LIGI YAILAMU YANGA KWENYE DABI YA KARIAKOO, KISA HIKI HAPA