Home Habari za michezo GAMONDI ATAMBA SIO MTU MMOJA MMOJA NI KIKOSI KIZIMA ETI……ISHU IKO HIVI

GAMONDI ATAMBA SIO MTU MMOJA MMOJA NI KIKOSI KIZIMA ETI……ISHU IKO HIVI

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesisitiza kuwa katika kikosi chake anataka kuona kila mchezaji anaweza kufunga mabao pale anapopata nafasi.

Katika misimu miwili iliyopita, Yanga ilimtegemea zaidi mshambuliaji Fiston Mayele ambaye ametimkia Pyramids Fc ya Misri

Wakati Mayele anaondoka wengi waliamini Yanga itayumba kwa sababu Mcongomani huyo alichangia karibu asilimia 80 ya mabao yaliyofungwa na Yanga.

Hata hivyo tangu ujio wa Gamondi ni kama falsafa ya timu hiyo katika ushambuliaji imebadilika wafungaji wakiwa wengi.

Gamondi ameeleza sababu kwa nini hapendi timu yake iwe tegemezi kwa mchezaji mmoja katika kufunga mabao.

“Ikiwa utakuwa unawategemea washambuliaji peke yake inakuwa rahisi kwa wapinzani kuwapa presha hao wachezaji na mwisho watakwama kukupa ushindi”

“Kila mchezaji anafunga awe ni beki, kiungo na hata washambuliaji nao wanafunga jambo ambalo ni zuri kwetu. Makosa yanayojitokeza tunaendelea kuyarekebisha lakini jambo muhimu kwetu kwa kiasi kikubwa tumeweza kukamilisha malengo yetu katika mechi zilizopita,” amesema Gamondi.

Katika orodha ya wafungaji ligi kuu ya NBC, washambuliaji Hafiz Konkoni na Kennedy Musonda kila mmoja amefunga bao moja wakati viungo Stephane Aziz Ki, Mudathir Yahya na Max Nzengeli kila mmoja amepachika mabao mawili. Wachezaji wengine waliofunga mabao ni Yao Kouassi, Pacome Zouzoua na Dickson Job.

SOMA NA HII  SAKHO ASEMA HAYA KWA MARA YA KWANZA TANGUA AONDOKE SIMBA