Habari za michezo
HUYU GAMONDI SASA NI HATARI NI DOZI JUU YA DOZI AFANYA HAYA KAMBINI
Staff Desk
September 29, 2023
10:36 am
Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi katika kuhakikisha anapata ushindi kwenye mchezo wao dhidi ya Al Merrikh, kesho Jumamosi ameonekana kuwaongezea dozi ya mazoezi wachezaji wake ambapo jana alionekana akiwakimbiza wachezaji wake kwa kasi mazoezini, wakizunguka uwanja.
Aidha, Gamondi alionekana kuwafanyisha mazoezi ya nguvu akilenga kuwaongezea stamina na kasi kuelekea kwenye mchezo huo utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Akizungumza, Gamondi alisema anataka kona wanacheza kwa kasi muda wote na kutowapa nafasi wapinzani wao.
“Tulikuwa na mfumo mwingine kwenye mchezo wetu wa kwanza wa ugenini, na mchezo wa marudiano pia tutakuwa na mfumo mwingine kabisa, mazoezi ninayowafanyisha wachezaji wangu ni katika kuhakikisha kikosi kinakuwa imara na tunafikia malengo yetu, nataka kucheza soka la kasi zaidi,” alisema Gamondi.
Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.