Habari za michezo
MASAUBWIRE ARUKA NA SIMBA, YANGA KISA HIKI HAPA
Staff Desk
September 29, 2023
10:41 am
Afisa Habari wa JKT Tanzania Masau Bwire, amesema sio sahihi kwa wadau wa soka la Bongo kuamini Simba SC na Young Africans ndizo zina haki ya kutwaa Ubingwa wa Tanzania Bara kila msimu.
Kwa sasa Young Africans wanatetea Ubingwa wa ligi hiyo baada ya kuutwaa msimu wa 2022/23 chini ya Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi, na sasa ipo chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.
Bwire amesema ushindani wa ligi unaipa timu yoyote kutwaa ubingwa, hivyo wale wanaofikiria ubingwa ni mali ya Simba SC na Young Africans pekee watashangazwa na matokeo watakayoyaona.
Bwire amesema: “Imekuwa kawaida wengi wanafikiria labda ubingwa ni mali ya Young Africans na Simba SC, eti hawa wanastahili kutwaa ubingwa, hapana, timu zote zinazoshiriki ligi zina hadhi ya kutwaa ubingwa na sisi tunaweza kutwaa ubingwa wa watu wakashangaa.
“Mwendo ambao tumeanza nao mashabiki usiwape mashaka, bado tuna nguvu ya kuendelea kupambana na kupata matokeo mazuri kwenye mechi zetu.”
Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.