Home Habari za michezo HATMA YA KRAMO KUJULIKANA WIKI HII…MADAKTARI WAFUNGUKA GONJWA HATARI LINALOMTESA…

HATMA YA KRAMO KUJULIKANA WIKI HII…MADAKTARI WAFUNGUKA GONJWA HATARI LINALOMTESA…

Habari za Simba

Majeraha ya mara kwa mara yanayomkumbwa winga mpya wa Simba SC Aubin Kramo yanazua maswali kwa mashabiki wa Simba SC juu ya mchezaji huyo alietazamiwa kuongeza kitu ndani ya Simba katika kampenui ya kusaka mataji 2023/24.

Lakini tangu kutua kwa Nyota huyo bado hajaweza kuonesha kile kilichotarajiwa na wengi kutokana na kuandamwa na majeraha.

Sasa Afisa Habari wa Simba Ahmed Ally ameweka wazi kuhusu hali ya majeraha ya mchezaji na hatua ambazo Simba itazichukua.

Akizungumza Ahmed anasema;

“Aubin Kramo anasumbuliwa na goti, huenda tatizo lake lilianzia ASEC lakini limekuja kujitokeza akiwa Simba. Majibu ya madaktari yatajulikana wiki hii, kama atafanyiwa operation au lah .. Madaktari wamesema kama tungeendelea kumchezesha huenda angepoteza career yake. Anasumbuliwa na mishipa nyuma ya goti”

SOMA NA HII  MIEZI MICHACHE BAADA YA KUTOKA SIMBA...GADIEL MICHAEL AFUNGUKA A-Z SIRI ZOTE ZA BOCCO..