Home Habari za michezo MAJERAHA YA KRAMO USHIRIKINA WAHUSISHWA, KAPOMBE ATAJWA

MAJERAHA YA KRAMO USHIRIKINA WAHUSISHWA, KAPOMBE ATAJWA

Habari za Simba

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kupitia runinga ya TV3, Boiboi Mkali, amefunguka kuhusu majeraha yasiyoeleweka ambayo yamekuwa yakiwakumba wachezaji wa Simba SC huku imani za kishirikina zikitajwa.

Boiboi amesema hayo kufuatia majeraha ya winga mpya wa Simba, Aubin Kramo raia wa Ivory Coast ambaye kila anapojaribu kurejea uwanjani amekuwa akipata majeraha na kubaki nje ya uwanja.

Kramo ambaye hajacheza mchezo wowote rasmi wa kimashindano akiwa na timu hiyo ambapo juzi aliumia wakati wa mchezo dhidi ya Ngome FC ikiwa ni siku chache baada kurejea uwanjani kutoka kwenye majeraha ya goti aliyoyapata mara tu baada ya kutua Simba.

“Wakati Shomary Kapombe alipokaanje kwa muda na kukosa kucheza katika kikosi cha kwanza kutokana na majereha. Baada ya kurejea kwenye kikosi na kufanyiwa interview na waandishi wa habari kuhusu majeraha aliyoyapata.

“Kapombe alisema akiwa mazoezi alikuwa anasikia maumivu, lakini akienda kupata vipimo Hospitali tatizo halionekani, mashabiki wengi walichukulia kwenye imani na kishirikina na mbaya zaidi wakamtuhumu mchezaji anayecheza katika nafasi moja na yeye,” amesema Boiboi.

SOMA NA HII  WIKI YA WANANCHI YANGA..TAREHE YATANGAZWA...KUPISHANA ANA SIMBA DAY KWA SIKU MBILI TU...