Home Habari za michezo MCHAMBUZI:- KAKOLANYA HAKUNA ALILOLIFANYA DHIDI YA ALGERIA…HATUKUONYESHA KIWANGO…

MCHAMBUZI:- KAKOLANYA HAKUNA ALILOLIFANYA DHIDI YA ALGERIA…HATUKUONYESHA KIWANGO…

Habari za Michezo

Tanzania imefanikiwa kufuzu fainali za AFCON 2023 usiku wa juzi baada ya kitoa sare ya bila kufungana na Timu ya Taifa ya Algeria katika Dimba la May 19, nchini humo.

Matokeo hayo yalizifanya Algeria kufikisha alama 16 akiwa kinara wa kundi na Tanzania alama 8 katika nafasi ya pili, alama hizi hazingeweza kufikiwa na timu yoyote kwenye kundi hilo, hivyo Uganda na Niger wakaaga mashindano dakika za lala salama.

Mchambuzi wa soka wa East Africa Radio, Michael Mwebe amedai kuwa kipa wa Stars, Beno Kakolanya alikuwa akijirusha ushahidi tu kwa sababu hakuna hatari yoyote ambayo Waarabu hao waliionyesha langoni mwake.

“Umaliziaji wa Algeria ulikuwa mbovu, mashuti yao hayakulenga lango, mara nyingi Beno Kakolanya alikuwa anaruka kwa mbwembwe za ushahidi kuna kipa golini wakati mpira uko mawinguni.

“Lakini hio sio issue, nadhani kikubwa na cha muhimu ni kuwa wachezaji wetu hawakupaniki kama ilivyokuwa ikitokea kwenye mechi nyingi zamani. Licha ya uwanja kuinama safu ya ulinzi haikufanya makosa ya kucheza faulo za kizembe za kuleta penati au Kadi nyekundu.”

“Ni sare iliyotokana na MENTALITY zaidi kuliko kiwango. Hatukuonesha ‘kiwango cha AFCON’ lakini tumeonesha UKOMAVU MKUBWA wa kupata matokeo kwenye mazingira magumu.

“Unahitaji UKOMAVU kuhimili kushikilia bomba Dar-Mwanza bila kuachia. Tumesafiri Dar-Mwanza kwa kusimama na tumefika salama. Huu ndio upambanaji and sometimes in life all you need is that fighting MENTALITY kwenye nyakati ngumu,” amesema @michaelmwebe.

SOMA NA HII  HAYA HAPA MAAJABU MATANO YA KIPA MBRAZIL WA SIMBA