Home Habari za michezo MCHAMBUZI:- KAPOMBE NA TSHABALALA WAMECHOKA MNOO…DUCHU HAMNA KITU MULE…

MCHAMBUZI:- KAPOMBE NA TSHABALALA WAMECHOKA MNOO…DUCHU HAMNA KITU MULE…

Habari za Simba

Mchambuzi wa Wasafi FM, Hans Rafael amesema kuwa Klabu ya Simba wanatakiwa kuwapumzisha mabeki wao wa pembeni, Mohammed Hussein Zimbwe’Tshabalala’ na Shomari Kapombe kwani wametumika muda mrefu bila kupumzika.

Hans amesema hayo wakati akichambua mapungufu ya kikosi cha Simba SC yaliyoonekana wakati wa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos ya Zambia na kutoa sare ya bao 2-2.

“Nilizungumza msimu uliopita kwamba Simba SC wanatakiwa waingie sokoni kutafuta fullback kiraka ambaye atacheza kulia na kushoto badala ya kutumia pesa nyingi kuchukua fullbacks wawili, nikamtaja Kouassi Attohoula Yao.

“Kinachotokea ni kwamba, fullbacks wa Simba, Zimbwe na Kapombe ni moja ya mabeki wazuri sana, wana uzoefu wa kutosha, wanakaba vizuri lakini wametumika muda mrefu sana zaidi ya miaka mitano mfululuzo. Ligi wanacheza wao, FA, Mapinduzi, CAFCL wanacheza wao, kifupi kila mechi wanacheza wao.

“Kwa hiyo unahitaji kuwa na backups au mtu ambaye atawaletea ushindani. Leo kapombe hata asipocheza vizuri anajua kesho atapangwa tena, hakuna presha anayoipata. Simba walitakiwa wawe na huyo mtu wa kuwapa usumbufu na ikiwezekana wapumzishwe acheze yeye.

“Simba hawakufanikiwa kufanya hivyo, wamemsajili Duchu, ni moja ya mabeki wazuri lakini sijaona kama ni bora ya kupambana na Kapombe. Inaonekana mwalimu bado hajawaamini yeye na Israel Mwenda hata dhidi ya Mtibwa hawapati nafasi.

“Kwa hiyo inaonekana kuna tatizo hilo na si la msimu huu tu, labda Simba waingie sokoni Januari watafute huyo mtu. Ni rahisi wapinzani kuwasoma Zimbwe na Kapombe kwa sababu wanatumika kila siku, anaweza kujua mapungufu ya Zimbwe na kumpa challenge. Gamondi anafanya hivyo kwa Yao na Kibwana, Lomalisa na Kibabage ndani ya Yanga SC,” amesema Hans.

SOMA NA HII  SIMBA: TUKIIFUNGA YANGA, UBINGWA NI ASILIMIA 100