Home Habari za michezo NGOMA AWAPATA JEURI VIONGOZI WA SIMBA, SIRI YAFICHUKA…YANGA WAPIGWA ZA USO

NGOMA AWAPATA JEURI VIONGOZI WA SIMBA, SIRI YAFICHUKA…YANGA WAPIGWA ZA USO

Habari za Simba SC

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’, amefichua kuwa wana uwezo mkubwa wa kuweza kusajili mchezaji yeyote wanayemtaka ndani ya timu hiyo.

Huku akishangazwa na kauli za wapinzani wao Yanga kudai waliporwa kiungo wa timu hiyo Fabrice Ngoma jambo ambalo halina ukweli wowote.

Try again ametoa kauli hiyo ikiwa baada ya kuwepo kwa maneno mengi juu ya kuhusu usajili wa Ngoma akitajwa kuwa Simba ilimpora kiungo huyo uwanja wa ndege wakati akitua nchini kwa ajili ya kumalizana na Yanga kabla ya kusaini Simba miaka. miwili akitokea Al Hilal ya Sudan.

Try Again afunguka kuwa, Simba inapotaka mchezaji yeyote haiwezi kumkosa na hakuna timu ambayo itamchukua mchezaji huyo kama ilivyofanya kwa Ngoma.

“Hizo stori kuwa tumemchukua uwanja wa ndege ni maneno tu, maana tulimaliza dili la Ngoma wiki moja kabla ya kutua hapa nchini.

“Kumpata Ngoma haikuwa ngumu kwa sababu ya uhusiano mzuri kati yetu na Al Hilal pia mchezaji husika alichagua kucheza Simba baada ya klabu zingine za nje ya Tanzania kuhitaji huduma yake.

“Ngoma ni mchezaji bora kwa Afrika, tumeweza kumnunua licha ya kukutana na vita vikubwa kutoka klabu zingine na siyo yeye hata usajili wa Willy Essomba Onana ulikuwa na changamoto kubwa siku ambayo tumemsajili.

“Kuna klabu ya Kaskazini mwa Afrika ikamtumia ujumbe kwenye simu yake ya mkononi na kumsumbua meneja wake kuachana na ofa yetu na kupewa pesa mara tatu zaidi tutakayompa, ulikuwa ugomvi mkubwa ingawa tuliweza kumbakisha,” alisema Try Again.

Try Again aliongeza kuwa soka la Tanzania sasa limekua sana, zamani wachezaji kutoka Magharibi mwa Afrika ikiwemo Ghana hawakutaka kucheza soka Simba lakini sasa hivi wachezaji wengi kutoka mataifa mbalimbali wanakuja kucheza.

SOMA NA HII  KAJULA:-" FREDY ATATUPELEKA NUSU FAINAL CAF....NIAMININI MIMI .... MO DEWJI ALTOA MIL 100 "

1 COMMENT

  1. Simba tunaanza na power dynamos kwa kuiondosha kwa sababu uwezo tunao na wachezaji tunao na tukimaliza tuna hamia kwa al ahly kwa kuiondosha super cup tunauwezo kwa sababu hapo juu kama nilivyo wambia kwa power dynamos