Home Habari za michezo RASMI SIMBA WAIANZIA MBALI POWER DYNAMOS….MBRAZILI AINGIZA JESHI KAMBINI…

RASMI SIMBA WAIANZIA MBALI POWER DYNAMOS….MBRAZILI AINGIZA JESHI KAMBINI…

Habari za Simba

KIKOSI cha Simba kinaingia kambini juzi (Jumamosi)na kutarajia kuondoka nchini Septemba 14, mwaka huu kuelekea nchini Zambia kwa ajili ya mchezo wa hatua ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba inaingia kambini kesho (jana) jijini Dar es Salaam na kucheza mechi ya kirafiki kabla ya kwenda Zambia kwenye mchezo wao dhidi ya Power Dynamos, utakaopigwa Septemba 16, mwaka huu katika uwanja wa Levy Mwanawasa.

Ahmed Ally alisema baada ya kufanya mazoezi takribani ya wiki mbili wachezaji wakitoka majumbani na kesho (Jumamosi) wanaingia kambini rasmi kujiandaa na mchezo huo kuhakikisha wanakuwa imara.

Alisema wachezaji wote wako vizuri na tayari kocha, Roberto Oliviera ‘Robertinho’, akitoa majukumu mazito kwa wachezaji wa timu hiyo akiwemo winga machachari Aubin Kramo.

“Wachezaji wote wapo sawa kutokana na kuendelea vizuri na program zake isipokuwa kwa wale ambao wapo kwenye majukumu za timu zao za taifa, tumekaa kwa muda mrefu tumeweza kufanya mambo mengi ya msingi kuelekea katika mchezo wetu wa Zambia na kitu kizuri tunaenda kucheza na mpinzani tunamfahamu vyema hatuhitaji kupuuzia kwa kuwa tunawafahamu.

matarajio yetu ni kuongeza nguvu kubwa katika mazoezi kutokana na majukumu ambayo kila mchezaji anayokueleka katika mchezo wetu ujao,” alisema Ahmed.

Aliongeza kuwa mpaka sasa timu yao ipo kwenye hali nzuri ambapo leo Jumamosi watachezaji wote wataingia kambini kabla ya kabla kuelekea Zambia Septemba 14, mwaka huu kwa ajili ya mchezo huo.

SOMA NA HII  NYOTA HAWA BONGO, UWEZO MKUBWA ILA NIDHAMU TATIZO KUBWA KWAO