Home Yanga SC YANGA WAZIDI KUJIIMARISHA, MWAMBUSI AANZA NA ISHU YA UFUNGAJI, ULINZI

YANGA WAZIDI KUJIIMARISHA, MWAMBUSI AANZA NA ISHU YA UFUNGAJI, ULINZI


KAIMU Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga, Juma Mwambusi ameendelea na mazoezi ya kikosi chake kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho.

Mwambusi amechukua mikoba ya Cedric Kaze ambaye alifutwa kazi Machi 7, 2021 kwa kile kilichoelezwa kuwa ni mwendo mbovu wa timu hiyo.

Katika mechi sita za Ligi Kuu Bara kwenye mzunguko wa pili Kaze alishuhudia sare nne, akishinda mechi moja na kichapo mechi moja kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Coastal Union, 

 Mwambusi amekuwa akiigawa Yanga makundi matatu kwenye mazoezi ya timu hiyo, ambapo kuna kundi kazi yake kukaba, kundi lingine kutengeneza nafasi za mabao na kupiga krosi huku kundi lingine likiwa na kazi ya kufunga tu.


Beki wa kati wa timu hiyo, Dickson Job, amesema kuwaMwambusi amekuwa akitengeneza uwiano wa timu kwa kufanya mazoezi ya mbinu ya kukaba na kufunga, zoezi ambalo limekuwa likifanyiwa kazi vizuri na wachezaji.


“Kimsingi kambi yetu inakwenda vizuri sana, kwa sababu kocha amekuwa akisisitiza timu kwenye kukaba, kutengeneza nafasi za mabao na kufunga kila wakati nafasi inapopatikana jambo ambalo tumekuwa tukilifanyia kazi mara kwa mara na kutoa matokeo chanya,” alisema Job.

 

Yanga wanafanya mazoezi kwenye uwanja uliopo Avic Town Kigamboni, sehemu ambayo pia wameweka kambi yao kwa muda wote tangu kuanza kwa msimu huu.


Chanzo: Championi


SOMA NA HII  BEKI WA AS VITA KUJIUNGA NA YANGA, MENEJA AELEZA WALIPOFIKIA