Home Uncategorized LICHA YA UCHOVU WA SAFARI, NAMUNGO WAIPIGA MKWARA KMC

LICHA YA UCHOVU WA SAFARI, NAMUNGO WAIPIGA MKWARA KMC

HITIMANA Thiery, Kocha Mkuu wa Namungo FC amesema kuwa uchovu kwa wachezaji unampa mashaka kidogo ila hesabu zao ni kushinda mechi yao leo dhidi ya KMC utakaochezwa Uwanja wa Majaliwa.

Februari 15, Namungo ilikuwa mkoani Shinyanga na ilimenyana na Mwadui FC ikaambulia pointi moja kwa sare ya kufungana bao 1-1.

Thiery amesema:”Wachezaji wanatumia muda mwingi kwenye safari ila kikubwa ambacho ninawaamini watapambana na kutafuta matokeo,”.

Namungo ipo nafasi ya tano ikiwa na pointi zake 37 itamenyana na KMC iliyo nafasi ya 16 na pointi 21.

SOMA NA HII  HAWA JAMAA NI WAZEE WA MIPENALTI, MBABE WAO HUYU HAPA