Home Habari za michezo SAIDOO, CHAMA, NA LUIS WAMTIA KIWEWE KOCHA WA POWER DYNAMOS….

SAIDOO, CHAMA, NA LUIS WAMTIA KIWEWE KOCHA WA POWER DYNAMOS….

Habari za Simba

BAADA ya kushinda mechi mbili za kirafiki dhidi ya Kipanga (3-0), na Cosmopolitan (5-1), Simba imeendelea na maandalizi ya mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos ugenini, lakini kocha mkuu wa Wazambia hao, Mwenya Chipepo ameshitukia kitu kwenye safu ya ushambuliaji ya Simba.

Chipepo aliyekuwa na kikosi cha Dynamos jijini Dar es Salaam, Agosti kwenye Tamasha la Simba Day, na kupoiteza kwa 2-0 dhidi ya Simba, ameshtushwa na mabadiliko yaliyofanyika ndani ya kikosi cha Simba katika siku 17 zilizopita.

Awali benchi la ufundi la Dynamos lilikuwa na faili zima la Simba lenye mechi nne za kwanza ambazo Mnyama alicheza msimu huu dhidi ya Singida na Yanga kwenye Ngao ya Jamii na zile za ligi dhidi ya Mtibwa Sugar na ile ya mwisho na Dodoma Jiji Agosti 20, lakini baada ya hapo Simba imebadilika jambo lililomfanya kocha huyo kuanza kuumiza kichwa upya atengenezeje timu.

Chipepo amesema kuwa alikuwa akitengeneza timu kwa kuijenga safu yake ya ulinzi kuwakabili, Saidi Ntibanzokiza, Jean Baleke, Kibu Denis, Moses Phiri na Clatous Chama lakini kuwa fiti kwa Luis Miquissone na kupona kwa, Kramo Aubin na Moses Phiri kumemchanganya.

“Tunatengeneza timu kutokana na mpinzani tunayekutana naye. Mwanzo tulikuwa tukiandaa mpango wa kucheza na Simba ambayo ilianza ligi lakini mapumziko haya yaliyotokea kupisha Kalenda ya FIFA, huenda yakawa na mabadiliko.

Kuna wachezaji wa Simba awali hawakuwa fiti lakini sasa wamerejea kikosini na naamini watakuwa kwenye mipango ya mwalimu kwani wamepata muda mrefu wa kujifua, sasa tunaenda kujiaanda upya kwaajili ya kuwakabili wote na naamini tutafanikiwa,” alisema Chipepo aliyewataja Saido na Luis kuwa wachezaji hatari zaidi Simba.

SOMA NA HII  AZAM FC AKILI KUBWA IPO HUKU