Home Habari za michezo TATIZO LA SIMBA LIKO HAPA

TATIZO LA SIMBA LIKO HAPA

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kutoka Wasafi Media, Nasir Khalfan amesema kuwa ndani ya kikosi cha Simba SC kuna tatizo ambalo limekuwa likisababisha timu hiyo kufungwa mabao licha ya kushinda michezo yao.

Khalfan amesema hayo kupitia Sport Arena ya Wasafi FM mara baada ya Simba Sc kutoa sare ya bao 2-2 dhidi ya Power Dynamos ya Zambia kwenye mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika na kudai kuwa uwiano wa timu kwenye kushambulia na kukaba ndiyo tatizo kubwa lilipo hivyo mwalimu Robertinho anatakiwa afanyie kazi eneo hilo ili kuimarisha kikosi chake.

“Matokeo ambayo wameyapata Simba mpaka sasa, bado hayajawatoa kwenye malengo yao ya msimu huu. Kwenye Ligi wameshinda mechi zao zote mbili, kwenye champions league wamepata sare ya bao 2-2 ugenini, wanarudi nyumbani wakiwa na mtaji wa mabao mawili ya ugenini.

“Matokeo yao yanaridhisha lakini ukiangalia namna ambavyo timu inacheza unaona kuna kutu hakiko sawa, haijakaa vile wanavyotamani timu iwe.

“Tatizo kubwa ni balance ya timu inavyotakiwa kuwa, kumiliki mpira imekuwa tatizo, kuna maeneo yanaonekana ni dhaifu. Mfano hizi mechi walizocheza inaonekana wapinzani wanapata mianya mingi ya kuishambulia Simba.

“Mechi ya kwanza ya Ligi dhidi ya Mtibwa uliona Lyanga alikuwa akitafuna mianya iliyokuwa inaachwa na wachezaji wa Simba na kuwafunga bao 2, mechi ya Dodoma imeonekana kuna kitu hakiko sawa hata mechi ya Power Dynamos hivyo hivyo.

“Mechi ya Power Dynamos kipindi cha kwanza Simba walionekana kuna vitu vingi hawavifanyi kwa usahihi, wapinzani wakawa wanapata mianya mingi ya kuwaona mabeki wa Simba. Mtu anatoka na mpira katikati ya uwanja mpaka anatoa pasi bao linapatikana hakuna mtu aliyemfanyia marking.

“Muundo wanaohitaji Simba kwa ajili ya kushambulia na muundo wanaohitaji kwa ajili ya kukaba, hiyo balance haipo.

“Washambuliaji walikuwa wanaonekana na madhaifu mengi, Kibu anapata mpira anakaa nao sekunde kadhaa hana wa kumpasia, Phiri naye hivyo hivyo anapata mpira lakini hana wa kumpasia mpaka aduni anauchukua.

“Simba watengeneze balance ya timu kuanzia ulinzi, katikati mpaka eneo la ushambuliaji. Inawezekana kocha Robertinho kuna wachezaji anahitaji kuwatumia lakini bado hajawaamini ipasavyo.

“Mtu kama Ngoma anatakiwa kuanza kwenye kikosi cha Simba sababu ana-contorl mechi, anapeleka mipira mbele lakini Robertinho inawezekana kuna kitu bado anakitafuta eneo la katikati ya uwanja,” amesema Nasir Khalfan.

SOMA NA HII  MKATA UMEME WA SIMBA LWANGA AKANA KUCHEZA RAFU