Home Habari za michezo SIMBA HAKUNA KUPOA, WAPITILIZA KAMA UTANI

SIMBA HAKUNA KUPOA, WAPITILIZA KAMA UTANI

Kikosi cha timu ya Simba kimerejea nchini jana Jumatatu, Septemba 18, 2023 wakitokea nchini zambia ambako walikwenda kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Power Dynamos ambapo walitoa sare ya bao 2-2.

Akizungumza leo, Meneja wa Habari na mawasiliano wa Kalbu ya Simba, Ahmed Ally amesema kuwa kikosi hicho kimeelekea kambini moja kwa moja kwa ajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Coastal Union utakaopigwa keshokutwa Alhamisi, Septemba 21, jijini Dar es Salaam.

“Moja kwa moja mara baada ya kurejea nchini tukitokea Zambia kwenye mchezo wa Ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos, vijana wetu wameingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Tanzania Prisons.

“Leo vijana watafanya recovery kwa ajili ya kuanza mikakati ya kuchukua alama tatu mbele ya Wagosi wa Kaya katika mchrzo huo wa raundi ya tatu wa Ligi,” amesema Ahmed Ally.

Simba wapo nafasi ya nne kwenye Ligi Kuu nyuma ya Mashujaa wanaoongoza Ligi, Yanga nafasi ya pili na Azam FC nafasi ya tatu.

SOMA NA HII  RUVU SHOOTING vs YANGA ...HAKUNA MBABE...MAYELE 'ACHEZEWA UNDAVA MWINGI' TENA...ASHINDWA KUTETEMA...