Home Habari za michezo WAFAHAMU WAARABU WALIOMSAJILI MSUVA….’MAMBO YAO NI KAMA YANGA TU’…

WAFAHAMU WAARABU WALIOMSAJILI MSUVA….’MAMBO YAO NI KAMA YANGA TU’…

Msuva Algeria

JS Kabylie au JSK ambayo amejiunga nayo mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva kwa mkataba wa miaka miwili ni klabu ya soka huko Algeria yenye makao yake makuu mjini Tizi Ouzou.

Klabu hiyo imepewa jina kutokana na eneo la kitamaduni, asili na la kihistoria ambalo ni nyumbani kwa watu wa Kabyle Berber wanaozungumza Kikabyle. Klabu hiyo ilianzishwa mwaka 1946 na rangi zake ni njano na kijani kama ilivyo rangi za Yanga.

Uwanja wao wa nyumbani, Hocine-AƃĀÆt-Ahmed, una uwezo wa kuchukua watazamaji 50,766. Klabu hiyo kwa sasa inacheza Ligi ya Algeria Professionnelle 1. Ndiyo klabu yenye mafanikio makubwa zaidi ya soka Algeria katika ngazi ya Afrika ikiwa na mataji saba ya Afrika.

JS Kabylie imeshinda taji la Ligue ya Algeria Professionnelle 1 mara 14, Kombe la Algeria mara tano, Kombe la Ligi ya Algeria mara moja na Super Cup ya Algeria mara moja.

Klabu hiyo pia imeshinda mataji kadhaa ya Afrika, likiwemo Ligi ya Mabingwa Afrika mara mbili, Kombe la Washindi wa Kombe la Afrika mara moja, Kombe la CAF mara tatu na Kombe la Super Cup la Afrika mara moja.

SOMA NA HII  TETESI ZA USAJILI SIMBA...MOHAMMED HUSSEIN KUSHUSHIWA VYUMA HIVI...BENCHIKHA ATOA KIBALI...