Home Habari za michezo POWER DYNAMO WALIFICHA SILAHA ZAO HAPA KUHUSU SIMBA

POWER DYNAMO WALIFICHA SILAHA ZAO HAPA KUHUSU SIMBA

Habari za Simba

Shabiki wa Klabu ya Simba, Aggy Danny maarufu kama Aggy Simba, amesema kuwa wapinzani wao kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa frika, Power Dynamos ya Zambia walificha baadhi ya wachezaji wao kwenye mchezo waliowaalika wakati wa sherehe za Simba Day, mwezi Agosti mwaka huu kwenye Dimba la Mkapa.

Simba wameanza safari leo kuelekea Zambia kuwafuata Power Dynamos kwa ajili ya mchezo huo utakaopigwa kwenye Dimba a Levy Mwanawasa, wakati Simba wakiwa na kumbukumbu ya kuifunga timu hiyo bao 2-0 kwenye mchezo wa kirafiki wa SImba Day.

Aggy amesema kuwa, Simba imejiandaa vyema kwa ajili ya kwenda kupata ushindi ugenini ili kujihakikishia kusonga mbele katika hatua ya makundi ya michuano hiyo.

“Tutaenda kukutana na Power Dynamos ambayo tumecheza nao kwenye Simba Day, wakati wanakuja Simba Day walikuwa wanajua kabisa wanaenda kwenye Champions League watacheza na timu fulani wakitoka watakutana na Simba.

“Kwa hiyo inawezekana pia walivyokuja hapa kwa Mkapa labda hawakutaka kujionesha wao wako vipi.

“Wanaweza wakawa walicheza wakaficha silaha zao ili kutuonesha kwamba wao ni wa kawaida kwa sababu walikuwa na imani kubwa maybe wangekutana na Simba (kwenye Champions League), hivyo hatuwezi kusema sana kwamba watakuwa ni wa namna gani,” amesema Aggy Simba.

SOMA NA HII  PUNA MAHELA KWA ODDS KUBWA ZA MERIDIANBET KWA MECHI ZA 16 BORA...LEO MZIGO UMESIMAMA NAMNA HII...