Habari za michezo

VIINGILIO VYA IHEFU vs YANGA HIVI HAPA

Staff Desk October 2, 2023 2:27 pm

Baada ya siku 309 tangu Yanga ifungwe na Ihefu mabao 2-1 Novemba 29 uwanja wa Highland Estate ulipo Mbarali mkoani Mbeya na kuharibu Unbeaten yao, Oktoba 4 watakutana tena katika uwanja huo tena kwa mechi ya Ligi Kuu.

Yanga ambao ni mabingwa watetezi Ligi Kuu na sasa wapo hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika bado hawajapoteza mchezo wowote Ligi Kuu msimu huu ikiwa kileleni kwa pointi 9 wakifunga mabao 11 bila kuruhusu bao.

Ihefu ipo nafasi ya 11 ikishinda mechi moja na kupoteza mbili tayari imetangaza kiingilio cha mechi hiyo itakayoanza saa 10:00 jioni kuwa ni Sh10,000 mzunguko na VIP Sh30,000.

LICHA YA SIMBA KUTINGA HATUA YA MAKUNDI ROBERTINHO AWAJIA JUU WACHEZAJI GAMONDI AWEKA WAZI SIRI HII YA YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply