Home Habari za michezo MAXI NZEGELI KWA YANGA SASA HIVI NI ZAIDI YA SHUJAA

MAXI NZEGELI KWA YANGA SASA HIVI NI ZAIDI YA SHUJAA

Habari za Yanga

Kama kuna mchezaji ambae sijamaliza kumzungumzia kwa sasa basi ni kiungo wa Yanga Max Nzengeli.

Yashasemwa mengi kuhusu huyu jamaa ila Max anateleza vizuri na mpira (gliding) kuwatoka mabeki nyie!

Iwe ni kwenye kimsitu cha wachezaji (akicheza 1,2 wakati mwingine), au hata akimtambuka mtu mmoja kwenye 1v1 yani yuko smooth sana!!!

Kama anateleza kwenye barafu hivi. Agility (wepesi wake wa mwili) na balansi yake akiwa na mpira ni kubwa sana.

Ni miongoni mwa wachezaji wepesi kama sio mwepesi zaidi kwenye kikosi cha Yanga kwa sasa.

Hatua ya Makundi waliyoingia Yanga ana mchango wake mkubwa sana.

SOMA NA HII  KUTOKA KUWA MKIMBIZI MPAKA KUSAJILIWA SIMBA SC....HAYA NDIO MAPITIO HALISI YA KIBU DENIS...