Home Habari za michezo BAADA YA UKIMYA MREFU….GOMES HUYU HAPA…SHAVU LAKE JIPYA NI ZAIDI YA SIMBA…

BAADA YA UKIMYA MREFU….GOMES HUYU HAPA…SHAVU LAKE JIPYA NI ZAIDI YA SIMBA…

Habari za Michezo

Baada ya mpango wa kujiunga na Singida Big Stars kukwama katika dakika za lala salama, kocha Didier Gomes da Rosa amepata ajira ya kuinoa timu ya taifa ya Botswana.

Kocha huyo raia wa Ufaransa, amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuinoa Botswana na jukumu lake kubwa litakuwa ni kuiongoza timu hiyo kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025, zitakazofanyika Morocco.

Habari za uhakika kutoka Botswana zinaeleza kuwa Gomes tayari ameshaanza kazi ya kuinoa timu hiyo na kibarua chake cha kwanza kitakuwa ni mechi mbili za kuwania kufuzu fainali Kombe la Dunia 2026, dhidi ya Msumbiji na Guinea ambazo watacheza mwezi ujao.

Kocha huyo ambaye bado hajatambulishwa rasmi na Chama cha Soka Botswana (BFA) katika majukumu yake hayo mapya. atasaidiwa na kocha wa zamani wa Township Rollers ya nchini humo, Romain Folz.

Da Rosa anakumbukwa nchini kwa kuiongoza Simba kuingia hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2020/2021, ambao iliondoshwa na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini kwa kufungwa mabao 4-3 katika mechi mbili baina yao.

Katika kipindi chake ndani ya Simba, Da Rosa alishinda taji moja la Ligi Kuu, Ngao ya Jamii pamoja na Kombe la Shirikisho la Azam.

SOMA NA HII  KUHUSU LOMALISA KUSEPA ZAKE YANGA...UKWELI UNAOPASWA KUJUA HUU HAPA...