Habari za Simba
Habari za michezo

SIMBA SASA HII NI FEDHEHA

Staff Desk October 31, 2023 10:22 am

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kutoka East Africa Radio, Samwel Rashid mwenyewe anajiita Wakanda Republic amesema kuwa Klabu ya Simba wanapaswa wabadilishe malengo yao badala ya kuishia robo fainali kila mwaka kwenye michuano ya Kimataifa.

Wakanda amesema hayo mara baada ya Simba kuishia kwenye hatua ya robo fainali ya michuano ya African Football League kufuatia kutolewa na Klabu ya Al Ahly ya nchini Misri.

“Simba inatakiwa wabadilishe malengo yao, au kuishia kwenye hizi hatua za robo fainali kwao isiwe mafanikio bali iwe ni fedheha, kwa sababu Standard unai-set kwa namna gani?

“Standard unai-set kwa kufika hatua fulani kwa mfululizo, umeshafika hatua ya makundi kwa mfululizo, umevuka, umeenda hatua ya robo fainali umeshaifika mfululizo, kwahiyo sasa utoke hapo uende sehemu inayofuata ya nusu fainali.

“Kwa sababu kama utaendelea kuishia hatua ya robo fainali ina maana haukui, kwamba wewe umedumaa kwenye hatua moja.

“Kwa sababu kama wewe una mfululizo wa kuishia hatua ya robo fainali, robo fainali, robo fainali ina maana umeishia sehemu kwamba uwezo wako ndio huo umedumaa kwenye hilo eneo,” amesema Wakanda Republic.

DABI YA KARIAKOO NGUMU KUMEZA,MANARA APATA KIGUGUMIZI AZIZ KI ATAMBA YANGA, ABEBA MILIONI 4 KIBOSI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply