Home Azam FC BANGALA KUIKOSA YANGA ISHU IKO HIVI

BANGALA KUIKOSA YANGA ISHU IKO HIVI

Kiungo Mkabaji wa kutoka DR Congo Yannick Bangala ameondolewa katika mipango ya Azm FC kuelekea mchezo wa Mzunguuko wasita wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Young Afrcans.

Miamba hiyo ya jiji la Dar es salaam itakutana Jumapili (Oktoba 22) katika Uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Beki huyo huyo aliyejiunga na Azam FC akitokea Young Africans, anaikosa Dar Dabi ya pili tangu ajiunge na timu hiyo, nyingine ilikuwa ile ya Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Ofisa Habari wa timu hiyo, Hashim Ibwe amesema kuwa mbali na kiungo huyo pia kuna na beki wa kati, Abdallah Kheir ‘Sebo’ ambaye alifanyiwa oparesheni ya goti.

Ameongeza kuwa benchi la ufundi na uongozi wa timu hiyo, wanafurahia kurejea kwa mshambuliaji wao Mzimbabwe, Prince Dube aliyepona majeraha yake ambaye hivi sasa anaongezewa mechi fitinesi ili awe fiti kwa mchezo huo.

“Bangala na Sebo ndio wachezaji pekee watakaokosekana katika mchezo wa Dar es salaam Dabi tutakaocheza dhidi ya Young Africans, lakini wachezaji wengine wote wapo fiti.

“Bangala alipata maumivu ya misuli katika mchezo wetu wa ligi dhidi ya Dodoma Jiji, lakini hivi sasa anaendelea vizuri na upo uwezekano mkubwa wa kurejea haraka uwanjani baada ya kupata nafuu.

“Mchezo wetu huu ni muhimu kupata ushindi, kwa lengo la kulipa kisasi cha kufungwa katika nusu fainali ya Ngao ya Jamii, uzuri wachezaji wapo katika morali kubwa ya ushindi,” amesema Ibwe

SOMA NA HII  MWAMBA KAGOMA KUSEPA NANI ATOKE SIMBA !?