Home Habari za michezo MNAOENDA KWA MKAPA LEO HILI LINAWAHUSU…ULINZI NI KAMA MECHI YA KOMBE LA...

MNAOENDA KWA MKAPA LEO HILI LINAWAHUSU…ULINZI NI KAMA MECHI YA KOMBE LA DUNIA..

Habari za Michezo

Mashabiki wengi wanaoendelea kumiminika katika uwanja wa Benjamin Mkapa wamekutana na kitu cha tofauti kama walivyozoea.

Leo Simba inashuka kumenyana na Al Ahly saa 12:00 jioni mchezo wa ufunguzi wa African Football League ambao unashirikisha timu nane bora Barani Afrika.

Iko hivi mashabiki wakifika katika mageti ya kuingia uwanjani wanatakiwa kuacha chupa zao za maji ya kunywa getini tofauti na ilivyozoeleka katka michezo mingi iliyopita.

Imekuwa jambo la kushtua lakini wameelewa baada ya kupewa maelekezo na polisi waliosimama vyema kuimalisha ulinzi wa raia na mali zao.

Hakuna aliyebisha baada ya kuambiwa kufanya hivyo walitekeleza na kuingia ndani kwa utaratibu mzuri.

Mbali ya hilo eneo la mageti ambao mashabiki usimama kwa ajili ya kuingia ndani ya uwanja limezungushwa vyuma ikiwa na lengo la kuepusha msongamano kutoka na ukubwa wa mchezo huu wa leo ulioteka soka la Afrika.

Licha ya kuwekewa vizuizi hivyo mashabiki wamekuwa watulivu na kufuata taratibu wakiingia kwa mstari.

Sasa ni saa saba mchana mtanange utaanza saa 12 jioni ambapo kila timu inahitaji matokeo katika dakika 90 za mchezo.

Mara baada ya mchezo huu wiki ijayo watarudiana nchini Misri na atakayemtoa mwenzake atakuwa na Kibali cha kusonga mbele

SOMA NA HII  KARIA AIBWAGA SIMBA KAMA MASIHARA