Home Habari za michezo KISA KARIAKOO DABI YANGA YAPIGWA FAINI…KULIPA MAMILIONI HAYA…WAFANYA KOSA HILI

KISA KARIAKOO DABI YANGA YAPIGWA FAINI…KULIPA MAMILIONI HAYA…WAFANYA KOSA HILI

Habari za Michezo leo

Timu ya Simba Sports Club imetozwa faini ya Sh. 1,000,000 (milioni moja) na Yanga Sports Club nao ikitozwa faini ya Sh. 5,000,000
(milioni tano) kwa kosa la kuingia kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa kupitia milango isiyo rasmi kuelekea kwenye mchezo wao wa Dabi ya Kariakoo, uliopigwa Aprili 20, 2024 na Yanga kuibuka na ushindi wa bao 2-1.

Taarifa iliyotolewa na bodi ya Ligi imesema kuwa, Yanga wametenda kosa hilo katika michezo minne iliyozikutanisha klabu hizo za Kariakoo ndani ya misimu minne kuanzia msimu wa 2021-2022, 2022-2023 na 2023-2024 ya Ligi Kuu.

Aidha, taarifa ya bodi ya Ligi imesema kuwa Yanga hawakutumia chumba cha kubadilishia nguo baada kukuta kuna harufu isiyo ya kawaida jambo lililomlazimu daktari wa mchezo kuchukua sampuli kwa ajili ya vipimo huku Yanga wakipewa eneo jingine kwa ajili ya kubadilishia nguo.

Kwa upande wa Simba wao walitumia chumba cha kubadilishia nguo katika kipindi cha kwanza lakini waliporejea mapumzikoni
hawakutumia chumba hicho.

SOMA NA HII  KAMWE:- SIMBA INA UONGOZI MAKINI NA IMARA...TUTAINGIA CHAKA...AWAPIGIA SALUTI WACHEZAJI SIMBA