Home Habari za michezo KISA SARE TATU…KAZE AWAAMBIA YANGA WAACHE KULALAMIKA LALAMIKA HOVYO…WANAWAHARIBU WACHEZAJI…

KISA SARE TATU…KAZE AWAAMBIA YANGA WAACHE KULALAMIKA LALAMIKA HOVYO…WANAWAHARIBU WACHEZAJI…


Kocha Msaidizi wa Yanga Sc, Cedrick Kaze raia wa Burundi amesema malalamiko amesema malalamiko ya baadhi ya mashabiki yanavunja moyo wachezaji wa timu hiyo.

Kaze amesema hayo jana Jumatatu, Mei 9, 2022 baada ya mchezo wao wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Tanzania Prisons ambao ulipigwa katika Dimba la Mkapa na kumalizika kwa sare ya bila kufungana.

Hii ni mechi ya tatu mfurulizo sasa kwa Yanga katika Ligi hiyo wakicheza bila kuibuka na ushindi ambapo hali hivyo imeanza kuibua mijadala kuwa huenda ndoto za ubingwa zikaanza kufifia kutokana na kupunguza kasi huku Ligi ikielekea mwishoni.

β€œMatokeo mabaya ni kweli yanaumiza hata sisi makocha hakuna anayefurahia kuona timu yake haipati matokeo mazuri, tunaumia sana lakini hatuna jinsi, cha msingi tunaangalia mechi zijazo tufanye vizuri.

β€œNajua wanaumia sana kuona timu haifanyi vizuri lakini wajue Mungu huenda kuna kitu kikubwa ametuandalia huko mbele, habari za kulalamika hadi kupitiliza sio vizuri zinatuvunja moyo wachezaji,” amesema Cedrick Kaze.

SOMA NA HII  YANGA YATENGA BILIONI 8.1 ZA CAF